عنوان المقالة:الفرق بين مورفيم النفي بين اللغة العربية واللغة السواحيلية Tofauti ya Viambishi Kanushi Kati ya Kiswahili na Kiarabu.‏
محمد امحمد محمد علي الطاهر | Mohammed Amohamned Mohameed Ali Taher | 15570
نوع النشر
رسالة ماجستير
المؤلفون بالعربي
محمد الطاهر
المؤلفون بالإنجليزي
Mohammed Taher
الملخص الانجليزي
Lugha katika jamii mbalimbali zimekuwa zikitofautiana kutoka eneo hadi eneo kutokana na athari za kijiografia. Utofautiano huo licha ya kupatikana kwenye mpangilio wa matamshi, huwepo pia kwenye sarufi zake. Wakimnukuu Pei na Ganor, Kihore na Wenzake (2003) wameifasiri sarufi kuwa ni ‘Sayansi ya muundo wa lugha pamoja na sheria na kanuni za matumizi yake ambayo kwa kawaida, hukubalika kwa watumiaji wake. Maana hiyo inatoa mwelekeo wa kubaini kwamba licha ya kila lugha kuwa na muundo wake, inayo pia sheria na kanuni za kimatamshi katika matumizi ya kila siku. Sarufi huhusisha vipengele vine vikuu ambavyo ni umbo-sauti (fonolojia), sarufi-maumbo (mofolojia), sarufi miundo (sintaksia), na umbo maana (semantiki)(Kihore na wenzake, 2003).Maneno katika lugha hujengwa kwa viambishi anuwai. Katika kuvitolea ufafanuzi Kihore (mtajwa) amesema: Ni mofimu zinazoambatanishwa kwenye mzizi wa neno ili kuwakilisha hali au dhana mbalimbali zinazofungamana na neno pamoja na mofimu hizo. Nafasi ya viambishi katika maneno hutegemea lugha husika. Katika lugha ya Kiswahili kwa mfano, viambishi hujitokeza mwanzoni au mwishoni mwa mzizi (Kihore, 2008). Kimsingi viambishi hujengwa kwa sauti moja au zaidi zenye kubeba jukumu maalum. Kwa mfano, katika Kiswahili kuna viambishi vya aina tofauti kama vile vya nafsi, njeo, urejeshi, vyenye kuonyesha hali katika umoja na wingi nk Kimaumbile yayo, viambishi hivyo vinaweza kuambatana pamoja na viambishi kanushi ili kujenga ukanushi wa neno. Ukanushi ni hali ya kukataa/kukana jambo. Ukataaji katika lugha hujitokeza katika hali na maeneo tofauti. Kwa mfano katika Kiswahili ukanushi unaweza kuwakilishwa na kiambishi kimoja au viwili kwenye neno. Mfano, ninaimba–siimbi, na amekuja–hajakuja. Ukanushi pia huweza kujitokeza kwenye neno zima lenye umbo la ‘si’.
تاريخ النشر
01/05/2013
الناشر
The Open University Of Tanzania
رقم المجلد
رقم العدد
رابط الملف
تحميل (246 مرات التحميل)
رابط خارجي
https://scholar.google.com.ly/citations?user=k0EI5YIAAAAJ&hl=ar
الكلمات المفتاحية
viambishi
رجوع